Kemikali
za sumu zilizoko katika tumbaku ya sigara huharibu DNA za mwili wa
binadamu dakika chache tu baada ya mtu kuanza kuvuta sigara. Kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, kemikali hizo zinazoitwa Polycylic
Aromatic Hydrocarbons (PAHs) husababisha DNA ziharibike na kuongeza
uwezekano wa mtu kupata kensa.
Katika uchunguzi huo watalamu walichukua
kemikali hizo katika miili ya wavuta sigara na kuzifanyia uchunguzi,
ambapo waligundua kuwa, kemikali za PHA hubadilika haraka mwilini na
kuwa sumu ambayo huharibu DNA baada ya kupita dakika 15 hadi 30 tangu
kuingia tumbaku katika mwili wa binadamu. Sumu hiyo hubadilisha seli
mwilini au kufanya mutation, kitendo ambacho huweza kusababisha kensa.
Wataalamu hao wanasema, kitendo hicho hufanyika kwa haraka sana kama
vile inavyoingizwa mada ya sumu kwenye damu kwa sindano.
Habari hii ni
tahadhari kwa watu wanaotaka kuanza kuvuta sigara, kwani takwimu
zinatuonyesha kwamba, watu 3,000 hufariki dunia kila siku umwenguni
kutokana na kensa ya mapafu, maradhi ambayo husababishwa kwa asilimia 90
na uvutaji sigara. Madhara ya kuvuta sigara kwa muda mrefu yanajulikana
na wengi, ambayo ni pamoja na magonjwa ya moyo na kensa mbalimbali,
lakini wataalamu wanatuasa ya kuwa, madhara ya sigara huanza pale tu mtu
anapoanza kupiga pafu ya kwanza na kuingiza moshi wa sigara mwilini.
Hivyo bado hujachelewa na unaweza kuacha sigara hii leo!
No comments:
Post a Comment