Vivimbe vyenye majimaji katika ngozi ya mkono wambele vinavyoundwa na kimelea cha homa ya konokono
Kichocho (pia schistosomiasis au bilharzia) ni ugonjwa ambao minyoo midogo aina ya schistosoma inaingia mwilini na kusababisha uwasho katika viungo mbalimbali unaosababisha homa, udhaifu, kuwasha kwa ngozi na baada ya muda zaidi damu kwenye kinyesi na maumivu tumboni.
Habari za kimsingi kuhusu kichocho.
- Kuna takribani watu milioni 200 duniani walioambukizwa na kichocho.
- Asilimia kubwa wanaishi Afrika penye maeneo ambako hadi nusu ya wakazi wote wameambukizwa.
- Hali ya ugonjwa inatokea polepole ambako wagonjwa mara nyingi hawana lawama kwa muda mrefu au kwa mwendo mkali.
- Utambuzi wake hufanyika kwa kuchunguza kinyesi (mavi, mkojo) au damu.
- Tiba kwa kawaida ni dawa la praziquantel. Kama ugonjwa haukuendelea kwa muda mrefu mno wagonjwa wanaweza kupona kikamilifu wakitibiwa.
Maambukizi ya kichocho yakoje?
- mnyoo mzima unatega mayai,
- mayai yakifika katika maji yanabadilika kuwa lava.
- lava zinatafuta konokono ya maji, zinaingia na kukomaa ndani ya konokono
- lava zilizokomaa zinatoka nje na kumtafuta binadamu, zikitoboa ngozi yake na kuingia katika damu.
- lava zinazunguka mwilini hadi kufikia maini, hapa zinakua kuwa minyoo wazima wenye urefu wa milimita 1-2 wanaokaa katika mishipa ya damu wamapotega mayai.
- mayai huvurugisha kinga ya mwili na kusababisha kuwaka kwa mishipa ya ndani ya mwili (yaani ugonjwa mwenyewe), yanaingia katika viungo vya mkojo au utumbo mpana yanapotoka tena mwilini.
Kwa hiyo maisha ya schistosoma na nafasi ya maambukizi huhitaji
- mwili wa kibinadamu (au kwa aina nyingine: pia ya wanyama)
- konokono ya maji
- mazingira ambako konokono zinastawi: maji ya bwaba au ziwa, penye mimea ya majini inayofaa kama chakula cha konokono
- watu wagonjwa wanakojolea kwenye maji au kuacha kinyesi chao mle
Kwa hiyo njia ya kuambukizwa ni kuingia katika maji penye konokono zilizoambukizwa. Siku hizi karibu kila ziwa au bwawa katika Afrika huwa na hatari ya kichocho; hatari inapungua katika mito yenye mwendo wa maji au katika sehemu ya maziwa makubwa ambako kuna pwani pana ya mchanga bila mimea iliyo chakula cha konokono.
Jinsi ya kuzuia na Matibabu ya Kichocho.
Taratibu wa kukinga dhidi ya maradhi haya ni pamoja na upatakanaji wa maji safi na upungufu wa idadi ya konokono. Katika maeneo ambako maradhi yanaambukiza zaidi, makundi ya watu walio wengi wanaweza kutibuliwa wakiwa pamoja wakati mmoja, kwa mara moja ya mwaka na dawa iitwao praziquantel. Taratibu huu unakusudia kupunguza idadi ya watu wanaoambukizwa na kwa hivyo kupunguza kuenezwa kwake maradhi yenyewe. Praziquantel ni dawa inayopendekezwa na Shirika la Afya Duniani kwa ajili ya wale wanaojulikana kuambukizwa.
ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOGU YETU...KARIBU TENA.
Dr Theobard M.Rwiza.
No comments:
Post a Comment