
Kidonda cha tumbo cha ndani kabisa.
Ugonjwa wa kidonda cha duodenamu (UKD), huitwao kwa kawaidakidonda cha tumbo, ni mpasuko katika sehemu ya juu ya tumbo, sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo, au mara chache umio. Kidonda tumboni huitwa kidonda cha tumbo huku kile kilicho kwenye sehemu ya kwanza ya matumbo kikiitwa kidonda cha duodenamu. Dalili ya kawaida sana ni kuamka usiku ukiwa na maumivu ya fumbatio la juu au maumivu ya fumbatio la juu ambayo hupungua unapokula. Maumivu haya mara nyingi huelezwa kuwa maumivu yanayochoma au yasiyo makali. Dalili zingine hujumuisha kupiga mbeu., kutapika, kupungukiwa na uzani, au kutokuwa na hamu ya kula. Takribani thuluthi ya watu walio wazee zaidi hawawi na dalili. Matatizo yanaweza kujumuisha kuvuja damu, kutoboka, na kuziba kwa tumbo. Uvujaji damu hutokea kwa asilimia 15 ya watu.
Je? Ugonjwa huu unasababishwa na nini? Na utawezaje kuutambua?
Visababishi vya kawaida hujumuisha bakteria, Filori helikobakta nadawa ya kumaliza inflamesheni isiyo na steroidi (NSAIDs).Visababishi vingine visivyo vya kawaida hujumuisha uvutaji tumbaku, mfadhaiko unaotokana na ugonjwa kali, Ugonjwa wa beseti, Sindromu ya ollinger-Ellison, Ugonjwa wa kroni na sirosisi ya maini, kati ya zingine. Watu waliozeeka zaidi huathirika zaidi na athari za NSAIDs. zinazosababisha kidonda Kwa kawaida utambuzi ukadiriwa kwa sababu ya dalili zinazodhihirika zinazodhibitishwa kwa endoskopiau barium swallow. Filori H. inaweza kutambuliwa kwa kufanya uchunguzi wa damu kutambua iwapo inakingamwili, uchunguzi wa pumzi wa urea, kuchunguza kinyesi ili kutambua dalili za bakteria aubiopsi ya tumbo. Hali zingine zinazosababisha dalili sawa hujumuishasaratani ya tumbo, ugonjwa wa moyo wa koronari, na inflamesheni ya sehemu ya juu ya tumbo au kibofu cha nyongo.
Epidemolojia na historia
Vidonda vya tumbo hupatikana katika takribani asilimia 4 ya watu.Takribani asilimia 10 ya watu hupata kidonda cha tumbo katika wakati fulani maishani mwao. Vilisababisha vifo 301,000 katika mwaka wa 2013 idadi iliyopungua kutoka kwa vifo 327,000 katika mwaka wa 1990.Maelezo ya kwanza ya kidonda cha peptisi kilichotobokayalikuwa katika mwaka wa 1670 katika PrincessHenrietta ya Uingereza. filori H. iligunduliwa kwanza katika mwaka wa 1981 na Barry Marshall na Robin Warren.
Uzuiaji na matibabu
Lishe haichangii sana katika kusababisha au kuzuia vidonda. Matibabu hujumuisha kutovuta sigara, kutotumiaNSAIDs, kutokunywa pombe, na dawa za kupunguza asidi ya tumbo. Kwa kawaida dawa inayotumika kupunguza asidi kwa kawaida ni proton pump inhibitor(PPI) au H2 blocker huku matibabu ya wiki nne yakipendekezwa hapo mwanzo. Vidonda vinavyosababishwa na filori H. hutibiwa kwa mchanganyiko wa dawa kama vile amoxicillin, clarithromycin, naPPI.Ukinzani wa antibiotikinti unazidi kuongezeka na hivyo matibabu yanaweza kutosaidia kila wakati. Vidonda vinavyovuja damu vinaweza kutibiwa kwa endoskopi, kwa upasuaji wa wazi unaotumika tu kwa kawaida pale ambapo haijafaulu.
ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOGU YETU..KARIBU TENA.
Dr Theobard M. Rwiza
No comments:
Post a Comment