Thursday, September 1, 2016
FAHAMU JINSI YA KUTUNZA NA KUULINDA UBONGO WAKO..
Baadhi ya viungo nyeti vya mwili vinaweza vikabadilishwa na wataalamu wa afya hospitalini na mtu akaendelea kuishi na bado akabakia kuwa mtu yuleyule.
Maendeleo ya teknolojia ya afya yamewezesha wagonjwa kuwekewa viungo bandia au vya watu wengine kama moyo, ini, figo, macho na kadhalika kwa mafanikio.
Neno mafanikio linamaanisha kuwa siyo tu kwamba wameendelea kuishi, lakini pia wameendelea kuishi wakiwa na haiba zao zilezile walizokuwa nazo awali.
Suala la ubongo ni tofauti kidogo. Kiufundi, inawezekana kumwekea mtu ubongo wa mtu mwingine na akaendelea kuishi. Tatizo ni kwamba, aliyewekewa ubongo hataendelea kuwa mtu yuleyule. Kihaiba atabadilika na kuwa kama yule mtu aliyekuwa anamiliki huo ubongo hapo awali!
Mathalani kama aliyewekewa ubongo alikuwa ni sheikh au padri na mtoa ubongo alikuwa jambazi, basi usishangae sheikh au padri huyo akitoka hospitali akabadilika na kuanza harakati za ujambazi!
Ubongo ni moja ya viungo vya lazima katika mwili. Bila ubongo uhai hauwezekani kwani utendaji kazi wa viungo vyote vya mwili na shughuli zinazofanywa na viungo hivyo hutegemea maelekezo kutoka katika ubongo.
Inakisiwa kuwa kwa wastani ubongo wa mwanadamu una kati ya seli bilioni 160 na bilioni 180. Kutokana na umuhimu wa ubongo, kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi kuulinda na kuuimarisha.
Mambo ya kufanya
Kunywa kiasi cha kutosha cha maji safi na salama kila siku ni moja ya mbinu muhimu za kulinda ubongo.
Kiasi cha kutosha mahitaji ni lita moja ya maji kwa kila kilo 25 za uzito wa mwili. Unapokuwa na upungufu wa maji, ubongo husinyaa na hivyo utendaji kazi wake hupungua.
Mbinu nyingine muhimu ni kunywa kiasi cha vijiko vitatu hadi vinne vya chakula vya mafuta ya nazi (ya kula) kila siku. Hii ni kwa sababu kadri umri wako unavyoongezeka ndivyo ubongo wako unavyoshindwa kutumia glukosi kama chanzo cha nishati.
Hii ni kutokana na seli za ubongo kujenga ubutu dhidi ya homoni ya insulini. Pamoja na kwamba uzito wa ubongo ni asilimia mbili tu ya uzito wote wa mwili, ubongo huo hutumia asilimia 20 ya nishati yote inayozalishwa mwilini.
Mafuta ya nazi ni mbadala wa glukosi kwa sababu hayahitaji insulini kutumiwa na seli za mwili ili kuzalisha nishati. Aidha mafuta ya nazi yamebainika kutoa kinga dhidi ya protini inayojulikana kama amyloid beta.
Kuwapo kwa protini hii husababisha uharibifu wa seli za ubongo zinazoitwa neurons ambazo zina jukumu maalumu la kusafirisha taarifa kati ya ubongo na maeneo mengine ya mwili.
Uharibifu wa neurons pamoja na mambo mengine husababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unaoitwa alzheimer.
Kama ilivyo kwa mafuta ya nazi, utafiti umebainisha kuwa kutumia kiasi cha kijiko cha chai kila siku pia kunatoa kinga mujarabu dhidi ya protini ya amyloid beta.
Kutumia kiasi cha gramu tatu za mafuta ya omega 3 kila siku ni mbinu nyingine ya kuupa ubongo siha inayohitajika.
Omega 3 ni mafuta yanayopatikana zaidi kwa samaki na viumbe wengine wa majini. Mbegu za mmea aina ya flax pia hutoa kiasi kikubwa cha mafuta ya omega 3.
Mafuta ya omega 3 yana faida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na kuimarisha ujazo wa ubongo. Tafiti zimebainisha kuwa matumizi ya omega 3 yanatoa kinga dhidi ya ugonjwa wa mfadhaiko na pia yanasababisha ongezeko la ujazo wa eneo la ubongo lenye tishu za rangi ya kijivu, hasa kwenye maeneo yenye seli zinazohusishwa na kuhisi furaha.
Kuulinda ubongo wako unahitaji pia kuacha mambo fulanifulani ambayo pengine unayapenda sana. Moja ya vitu unavyotakiwa kuachana navyo ni matumizi makubwa ya dawa, vinywaji au vyakula vyenye kiambata cha aluminiamu. Tafiti zimebainisha kuwa aluminiamu ni madini yanayosababisha uharibifu wa seli za ubongo.
Punguza matumizi ya pombe, sigara na piga marufuku matumizi ya dawa za kulevya. Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya hupunguza uwezo wa ubongo katika kufanya kazi zake kwa ukamilifu.
Baadhi ya wanaotumia dawa za kulevya ni rahisi kupoteza uwezo wao wa kujitambua na hata kuishi na jamii.
Ni vema pia kupunguza matumizi ya viuavijasumu (antibiotiki) vya kundi la fluoroquinolones. Pamoja na kwamba hivi ni viuavijasumu vyenye nguvu sana, na vinaweza kukukinga dhidi ya maambukizi ya bakteria hatari, hasa ikiwa umefanyiwa upasuaji, lakini viuavijasumu hivi vinahusishwa na uharibifu wa seli za akili, mishipa ya fahamu na maeneo mengine ya mwili.
Maeneo hayo ni kama vile tumbo, moyo, mifupa, macho, masikio na viungio vya misuli na mifupa. Inashauriwa pia kuachana na matumizi ya dawa za kupunguza lehemu mwilini za kundi la statins.
Dawa hizi zimebainika kusababisha madhara kwa mwili ikiwa ni pamoja na kusababisha uharibifu katika seli za ubongo zinazohusika na kumbukumbu, kusababisha kisukari cha ukubwani na kusababisha uharibifu wa misuli.
Unashauriwa pia kuachana na matumizi ya dawa za meno zenye floridi. Hii ni kwa sababu floridi ni madini yanayojulikana kuwa yanasababisha uharibifu wa seli za ubongo na mishipa ya fahamu.
Unashauriwa kuacha kutumia maji yenye floridi kwa ajili ya kuwezesha yawe safi na kutengenisha na vitu kama udongo na taka nyingine. Kama uwezekano upo tumia maji yaliyochujwa. Vichujio vya asili kama mchanga vina uwezo wa kuondoa taka mbalimbali kwenye maji ya kunywa ikiwa ni pamoja na mabaki ya dawa za kusafishia na kutakatishia. Dawa nyingi za kusafishia maji zina kiambata cha aluminiamu ndani yake na yale maji yaliyotakatishwa yanaweza kuwa na floridi. Mwisho funga kula mara kwa mara. Tafiti zinaonyesha kuwa ukarabati katika seli za ubongo hufanyika tu pale inapokuwepo homoni ya ghrelin. Aidha tafiti zinaonyesha kuwa homoni ya ghrelin huzalishwa na mwili pale tu tunapokuwa na njaa.
Hii ina maana kuwa unapokuwa umeshiba muda wote mwili hauzalishi ghrelin na kama haizalishwi basi ukarabati wa seli za ubongo haufanyiki
ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOGU YETU...KARIBU TENA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment