Tangazo

Tangazo

TIGO 4G

AIRTEL TANZANIA

Tembelea Tabibu wa kweli hapa Kila siku kufahamu magonjwa mbalimbali ya binadamu,vipimo vya kitabibu na ushauri wa kitaalamu

Monday, August 15, 2016

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION): SEHEMU YA PILI.....FAHAMU KWA UNDANI ZAIDI.

Shinikizo la juu la damu ni nini?
Shinikizo la juu la damu hutokea pale damu inaposukuma kuta za ateri kuongezeka hivyo kusababisha moyo kufanya kazi kubwa kuliko kawaida. Moyo kazi yake ni kusukuma damu katika ateri ambapo kutoka hapo inaelekea kwenye mwili mzima wa binadamu lakini kwa mtu mwenye shinikizo la juu la damu husababisha moyo ufanye kazi ya ziada ambayo hupelekea kukomaa kwa kuta za ateri au kufeli kwa moyo kabisa.
Jinsi ya kutambua una Shinikizo la juu la damu
Tofauti na magonjwa mengine, mtu anaweza kuwa na Shinikizo la juu la damu bila kuwa na dalili ya aina yoyote. Ila kuna dalili ndogo ndogo ambazo zinaweza kukujulisjha kuwa upo salama au una ugonjwa huu.
Ila kwa kufanya vipimo na kufutilia nyendo za mwili wako mara kwa mara unaweza ukazuia kifo cha ghafla. Kucheki presha ya damu yako mara kwa mara kunaweza kukakusaidia kujua kuwa una tatizo hili,
Kipimo cha presha ya damu ina namba mbili, ya juu (nyumereta) na ya chini (dinomineta). Namba ya juu inajulikana kama Sistoliki (Systolic) na ya chini hujulikana kama Dayastoliki (Diastolic).
Kipimo cha presha ya damu kinachosoma 120/80 ni cha kawaida kwa binadamu ila kipimo kinachosoma kati ya 120/80 na 130/89 anakuwa yupo katika dalili za mwanzo za Shinikizo la juu la damu na kama hatua hazitachukuliwa mapema basi anaweza akapata Shinikizo la juu la damu. Kipimo chochote kinachosoma zaidi ya hapo huashiriwa kuwa mtu ana tatizo la Shinikizo la juu la damu.
Ila, kwa watu wazima kipimo cha 140/90 huashiria Shinikizo la juu la damu. Hivyo inashauriwa kuchukua vipimo vya presha ya damu mara kwa mara ili kutambua, kuzuia au kupunguza hatari za Shinikizo la juu la damu.
Sababu za Shinikizo la juu la damu
Shinikizo la juu la damu limegawanyika katika sehemu mbili:
1. Shinikizo la juu la damu la msingi: Aina hii ya Shinikizo la juu la damu haina sababu inayoeleweka na mara nyingi inaweza kusababishwa na mazingira, jenetiki (Ugonjwa wa familia) au umri mkubwa. Asilimia kubwa ya watu wanaopata Shinikizo la juu la damu huwa katika kundi hili.
2. Shinikizo la juu la damu la sekondari: Aina hii mara nyingi husababishwa na magonjwa mengine ambayo yapo katika mwili wa binadamu. Kwa mfano, mara nyingi aina hii ya Shinikizo la damu huweza kuwatokea wanawake wakati wa ujauzito. Mara nyingi aina hii ya Shinikizo la juu la damu huona pale sababu inapotibiwa.
Sababu zingine za Shinikizo la juu la damu
1. Matumizi ya kilevi kupita kiasi: Matumizi ya kilevi kupita kiasi yanaweza kusababisha Shinikizp la juu la damu, na mara nyingine kuongeza uzito wa mtumiaji ambayo pia ni chanzo cha tatizo hili.
2. Dawa za Kulevya: Madawa ya kulevya kama Cocaine, Heroine na mengine mengi huweza kumsababishia mtumiai tatizo la Shinikizo la juu la damu.
3. Madawa ya kawaida: Matumizi ya madawa ya kawaida kupita kiasi kama, dawa za kichwa, kuzuia mimba, zenye kafeini pia huweza kusababisha Shinikizo la damu.
4. Fetma (Obesity): Fetm au unene kupita kiasi ni chanzo kikubwa cha Shinikizo la juu la damu, Uwepo wa mafuta kupita kiasi katika mwili wa mtu mwenye Fetma unasababisha uhitaji mkubwa wa nutirisheni na oksijeni kusababisha moyo kufanya kazi zaidi ili kufanikisha hili hivyo kusababisha Shinikizo la juu la damu.
5. Aina ya maisha: Kutokufanyisha mwili wako azoezi pia kunaweza kusababisha Shinikizo la juu la damu.
6. Mlo mbovu: Mtu mwenye tabia ya kula chakula chenye chumvi na mafuta mengi husababisha Shinikizo la juu la damu
7. Uvutaji wa Sigara: Tabia ya kuvuta sigara huepekea kufanya ateri kuwa nyembamba na kuta zake kuwa ngumu hivyo kusababisha moyo kufanya kazi zaidi katika kusukumiza damu mwilini.
8. Umri: Kadri umri unayoongezeka ndivyo hatari ya kupata Shinikizo la juu la damu inavyoongezeka pia
9. Ukosefu wa Vitamini: Ukosefu wa Vitamini D mwilini huweza kusababisha Shinikizo la juu la damu
Jinsi ya kupunguza madhara ya Shinikizo la juu la damu bila madawa
Shinikizo la juu la damu linaweza kupunguzwa au kuponywa kabisa kwa kuchukua hatua kadhaa za kupunguza chanzo cha ugonjwa huu. Baadhi ya njia za kupunguza madhara au kuponya Shinikizo la juu la damu bila madawa ni:
1. Punguza uzito: Kama una uzito kupita kiasi au una Fetma, kupunguza uzito kwa njia tofauti kunaweza kukusaidia sana katika kuponyesha Shinikizo la juu la damu.
2. Ingiza mazoezi katika ratiba yako: Kuufanyisha mwili wako mazoezi ya mara kwa mara unaweza kuponya Shinikizo la juu la damu. Hakikisha unafanya mazoezi hata dakika 30 kila siku.
3. Boresha ulaji wako: Hakikisha unatumia matunda, mboga mboga, potasiam vile vile punguza kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha Cholesterol na Chumvi.
4. Punguza matumizi ya pombe: Pombe ni chanzo kikubwa cha Shinikizo la juu la damu hivyo unatakiwa kupunguza au kuacha kabisa.
5. Acha Kuvuta Sigara: Kama ni mvutaji wa sigara, unashauriwa kuacha kabisa kwani sigara huongeza Nikotini kwenye damu ambayo huathiri ateri hivyo kusababisha Shinikizo la juu la damu.

ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOG YETU...KARIBU TENA.
    Dr Theobard M.Rwiza.


No comments:

Post a Comment