Tangazo

Tangazo

TIGO 4G

AIRTEL TANZANIA

Tembelea Tabibu wa kweli hapa Kila siku kufahamu magonjwa mbalimbali ya binadamu,vipimo vya kitabibu na ushauri wa kitaalamu

Sunday, December 31, 2017

MADHARA YA UNENE...

Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara makubwa kiafya hata vifo.

Unene hupimwa kwa kutumia kipimo kinachotambulika kitaalamu kama BMI (yaani uzito kwa Kilogram kugawa kwa urefu kwa mita mara mbili).

Tatizo la unene uliopindukia huweza kusababisha mhusika kutengwa katika jamii, kubaguliwa, kudhihakiwa hata kunyanyapaliwa hivyo kuleta madhara kisaikologia kwa mgonjwa.

Sababu za unene uliopindukia ni pamoja kurithi. Mtoto aliyezaliwa na wazazi wanene,ana asilimia 80 ya kuwa mnene,aliyezaliwa na wazazi wembamba, ana asilimia 10 ya kuwa mnene.

Utamaduni na ukosefu wa nidhamu katika vyakula, pia unachangia unene uliopindukia.

Mfano; kuna ongezeko kubwa la watoto na vijana wanene kwa sasa mijini kuliko vijijini.

Madhara yaletwayo na unene uliopindukia ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na kulika kwa jointi hasa za miguu, maumivu kiunoni na katika nyonga, shinikizo la damu,kisukari, pia kukosa usingizi kutokana na kubanwa kwa hewa.

Mengine ni athma, kiungulia, mafuta mengi mwilini, magonjwa ya moyo na moyo kushidwa kufanya kazi na mawe katika kibofu cha nyongo.

Wagonjwa hujikuta wakishindwa kufanyakazi vyema ili kujipatia kipato, hivyo kuwa tegemezi, kunyanyapaliwa pia huleta matatizo ya kisaikologia kama nilivyoeleza awali.

Matibabu ya ugonjwa huu ni pamoja na kubadili mfumo na aina ya maisha. Hii ni pamoja na kuwa na nidhamu katika chakula na kufanya mazoezi.

Ni wazi kwamba wazazi na watoto wanaoishi mjini, wanakabiliwa na tatizo hili, kutokana na maisha ya mfumo mgando ( kula kazi bila jasho-kulala, au kula-kusoma-kulala).

Dawa pia zina patikana na zinasaidia kupunguza uzito walau kwa asilimia 10 kwa mwaka, lakini hufanyakazi vyema iwapo mfumo wa maisha utabadilishwa.

Matibabu ya muda mrefu ya tatizo hili na ambayo husaidia mgonjwa kwa kiwango kikubwa ni kufanyiwa upasuaji. Upasuaji katika tumbo ndiyo tiba mwafaka kwa unene uliopindukia.


 KARIBU TENA TABIBU WA KWELI.
Read more »


SARATANI YA MATITI (BREAST CANCER): VISABABISHI,DALILI NA TIBA YAKE...


Kansa ya matiti ni aina ya kansa inayojitokeza toka tishu za matiti hasa mirija myembamba inayopitisha maziwa. Ugonjwa huu (Saratani ya matiti) hutokea kwa binadamu na mamalia wengine. Idadi ya wanaume wanaopatwa na kansa ya matiti ni ndogo sana ikilinganishwa na ya wanawake.
Ulimwenguni pote, kansa ya matiti hubeba asilimia 29 nukta tisa ya kansa zote kwa wanawake.
Licha ya maendeleo ya kitiba, bado kansa ya matiti ndiyo kansa inayosababisha vifo vingi zaidi vya wanawake.
Nchi zilizoendelea za Amerika Kaskazini na Ulaya Magharibi ndizo zenye idadi kubwa zaidi ya watu walio na kansa, lakini idadi ya wanawake walio na kansa ya matiti inaongezeka katika bara la Asia na Afrika ambako kwa kawaida kumekuwa na idadi ndogo kiukweli.
Idadi ya wanaokufa kati ya wale wanaogundulika kuwa na ugonjwa huo huko Asia na Afrika ni ya juu kwasababu kansa hiyo haigunduliwi mapema. Wagonjwa wengi huja ikiwa tayari imeenea sana.
Kansa ya matiti huanza wakati ambapo chembe moja inajigawanya haraka sana isivyo kawaida na bila utaratibu, na hatua kwa hatua inafanyiza uvimbe.
Uvimbe unakuwa kansa wakati chembe zake zinapovamia tishu nyingine. Uvimbe fulani unaweza kuchukua miaka kumi hivi kabla ya kugunduliwa.
VIHATARISHI/VISABABISHI
Hatari ya kupatwa na kansa hiyo huongezeka dadiri umri unavyosonga. Asilimia 80 hivi ya wanawake wenye kansa ya matiti wana umri unaozidi miaka 50.
Lakini jambo linalofariji ni kwamba kansa ya matiti ni mojawapo ya kansa zinazoweza kutibiwa kwa urahisi.
Watakao tibiwa kabla ya kansa hiyo kuenea wanaweza kuishi muda mrefu kwa ukawaida.
Visababishi vya kansa ya matiti bado ni fumbo.
Baadhi ya wanasayansi wanaamini kwamba kansa ya matiti hutokana na hatua nyingi tata ambazo huanza wakati ambapo chembe fulani ya urithi yenye kasoro inapofanya chembe zitende kwa njia isiyo ya kawaida, yaani, zigawanyike kwa kasi sana, zishambulie tishu nyingine na kuepuka kuharibiwa na mfumo wa kinga, kisha pole pole chembe hizo zinashambulia na kuharibu viungo muhimu vya mwili.
Jambo lingine linalohusishwa na kansa ya matiti ni homoni ya estrojeni ambayo huenda inachochea aina fulani za kansa hiyo.
Kwa hiyo, mwanamke anaweza kupatwa na kansa hiyo ikiwa alianza kupata hedhi mapema maishani au ikiwa aliacha kupata hedhi akiwa amechelewa isivyo kawaida, ikiwa alipata mimba ya kwanza umri wake ukiwa umesonga au ikiwa hakuwahi kupata mimba, au ikiwa alipata matibabu ya kurudisha homoni fulani mwilini.
Kwa kuwa chembe za mafuta hutokeza estrojeni, huenda wanawake walionenepa kupita kiasi waliofika umri wa kuacha kupata hedhi na hivyo ovari zao hazitokezi tena homoni, wakawa katika hatari ya kupatwa na kansa hiyo.
Pia watu walio na viwango vya juu vya insulini na watu walio na viwango vya chini vya homoni ya usingizi inayoitwa melatonia kama vile watu wanaofanya kazi usiku, wako pia katika hatari ya kupatwa na kansa hiyo.
Uvutaji wa tumbaku umeonekana kuongeza hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti, kiwango kikubwa cha tumbaku iliyovutwa na kuanza kuvuta tumbaku katika umri mdogo hufanya hatari kuongezeka zaidi.
Mionzi na kemikali za viwandani huongeza hatari ya kansa ya matiti. Kemikali kama polychlorinated biphenyls, polycyclic aromatic hydrocarbons na dawa za kuulia wadudu huchangia kutokea saratani hiyo.
DALILI
– Uvimbe wowote au kuongezeka kwa unene wa ngozi kwenye makwapa au titi.
– Umajimaji wowote unaotoka kwenye chuchu ambao si maziwa.
– Mabadiriko yoyote ya rangi au ngozi ya titi.
– Chuchu iliyodidimia kwa njia isiyo ya kawaida au inayowasha.
UCHUNGUZI KUJUA KAMA NI KANSA
Ili kuchunguza ikiwa uvimbe una kansa sindano nyembamba hutumiwa kutoa tishu kutoka kwenye uvimbe huo na kufanyiwa uchunguzi.
MATIBABU
Uvimbe ukiwa na kansa hufanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe huo na tishu zinazozunguka titi. Upasuaji husaidia kuonyesha uvimbe ulipofikia (ukubwa, aina na kuenea kwake) na kuchunguza uvimbe unakua upesi kadiri gani.
Chembe zenye kansa zinaweza kutoka kwenye uvimbe na kusafiri kupitia mfumo wa damu au mfumo wa limfu na kuanza kukua tena mahali pengine mwilini.
Kuenea kwa kansa hadi kwenye viungo na tishu muhimu kama vile ubongo, ini, uboho wa mfupa au mapafu ndio hufanya ugonjwa huo uwe hatari.
Hivyo baada ya upasuaji, wagonjwa wengi hupata matibabu mengine ambayo yatazuia kansa isirudi na kuenea.
Kwasababu ya maendeleo katika matibabu ya kansa ya matiti, kumekuwa na matibabu mbalimbali ikitegemea umri, afya historia ya kansa katika familia, na aina ya kansa.
Wanasayansi wanajifunza mambo mengine kuhusu kansa kutia ndani kuelewa ni kwa nini kansa huenea, kudhibiti chembe za kansa ambazo haziharibiwi kupitia matibabu ya kemikali, kuzuia kugawanyika kwa chembe na kutibu kila uvimbe kwa njia hususa.

ASANTE KUTEMBELEA BLOGU YETU..KARIBU TENA
Read more »


HOMA YA MAPAFU(PNEUMONIA): FAHAMU CHANZO CHAKE,DALILI,JINSI INAVYOENEZWA,UCHUNGUZI NA VIPIMO,MATIBABU NA NAMNA YA KUIZUIA..

.


A black and white X-ray picture showing a triangular white area on the left side. A circle highlights the area.


Homa ya mapafu(Pneumonia): ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu. Ni ugonjwa ambao unaua watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea duniani. Inakadiriwa kwamba watoto karibu milioni 1.6 walio chini ya miaka 5 wanakufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu. Kutokana na vifo vingi vinavyotokana na homa ya mapafu tarehe 12 ya mwezi wa Novemba kila mwaka imefanywa kuwa siku rasmi ya homa ya mapafu duniani, ambapo nembo ya siku hiyo ni nguo za rangi ya bluu.

Muundo wa Mapafu
Mapafu yanajumuisha mirija mikubwa ya hewa (bronchi) ambayo hugawanyika kufanya mirija midogo zaidi ya hewa (bronchioles), ambayo nayo hutengeneza vifuko vidogo vidogo ya hewa (alveoli). Vifuko hivi vidogo vya hewa (alveoli) vina mishipa ya kupitisha damu (capillaries) ambayo husaidia kuchuja na kusafirisha hewa safi ya oksijeni tunayovuta kuingia kwenye damu na hewa chafu ya ukaa (kaboni dioksidi) kuondolewa kwenye damu na kuingizwa kwenye mapafu tayari kwa kutolewa nje ya mwili.
Kwa kawaida vifuko hivi vidogo hujaa hewa muda wote tayari kwa kusafirishwa. Inapotokea mtu akapata homa ya mapafu, vifuko hivi hujaa maji au usaha hivyo kuathiri upitishaji wa hewa safi kwenye damu na kusababisha tatizo la kupumua.

Homa ya mapafu husababishwa na nini?
Kuna aina kadhaa ya vimelea ambao vinaweza kusababisha maambukizi ya mapafu. Vimelea hivi hujumuisha bakteria, virusi, parasite na fangasi.Vimelea hawa hushambulia mwili wa binadamu kulingana na umri na kinga ya mwili. Kwa mfano, bakteria wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wachanga ni tofauti na wale wanaosababisha ugonjwa huo kwa watoto wakubwa.
Baadhi ya vimelea wa bakteria wanaoshambulia watoto ni pamoja na Streptococcus pneumoniae ambao ni aina ya bakteria wanaoongoza kusababisha homa ya mapafu kwa watoto. Wapo pia Haemophilus influenzae aina b (Hib) ambao ni aina ya pili ya bacteria walio maarufu zaidi kwa kusababisha ugonjwa wa homa mapafu kwa watoto. Staphylococcus aureus ni aina nyingine ya bacteria ambao hushambulia zaidi watoto wachanga. Kuna pia Group B streptococci ambao pia hushambulia zaidi watoto wachanga.
Kwa upande wa virusi, virusi wa aina ya Respiratory syncytial virus ndiyo wanaoongoza kwa kusababisha homa ya mapafu kwa watoto.
Aidha, vimelea wa Pneumocystis jiroveci ambao kwa sasa huwekwa kwenye kundi la parasite ni maarufu zaidi miongoni mwa parasite wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wenye upungufu wa kinga mwilini hususani watoto wenye VVU.
Aina nyingine za bakteria ambao hushambulia zaidi watoto wakubwa ni pamoja na Mycoplasma pneumonia naChlamydia pneumonia.

Jinsi Homa ya Mapafu inavyoenezwa
Kuna namna nyingi za kuenea kwa homa ya mapafu. Kwa kawaida, virusi na bacteria hupatikana katika sehemu ya juu ya mfumo wa njia ya upumuaji (upper respiratory tract). Inapotokea kinga ya mwili ya mtoto imeshuka kwa sababu yeyote ile, vimelea hivi huweza kusambaa na kufika mpaka sehemu ya chini ya mfumo wa njia ya upumuaji (lower respiratory tract) na hatimaye kushambulia mapafu. Hali kadhalika, vimelea hawa wanaweza kuenea kwa njia ya damu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla ya kuzaliwa yaani kipindi cha mimba.
Dalili za ugonjwa wa homa ya mapafu
Dalili za vichomi au homa ya mapafu kwa watoto hutegemea na umri wa mtoto. Kwa watoto wadogo, dalili za awali zinaweza kuwa homa kali pamoja na mtoto kuhangaika na kunyong’onyea. Watoto wanaozaliwa wakiwa na uambukizi wa bacteria aina ya Streptococcus kundi B wanaweza kuwa na homa na kupumua kwa shida. Wakati mwingine mtoto anaweza kuwa na dalili ambazo si maalum (no-specific symptoms) kama vile kuhangaika na kushindwa kunyonya au kula vizuri bila kuwa na dalili yeyote ya kushindwa kupumua. Hali hii inaweza kutokea kwa mtoto wa umri wowote ule. Dalili za kawaida za homa ya mapafu ambazo huwapata karibu watoto wote wanaoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na:
homa
Kuhisi baridi
kikohozi
Kupumua kwa haraka kuliko kawaida
kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua
Mbavu za mtoto kuingia ndani wakati wa kupumua
maumivu ya tumbo
kupoteza hamu ya kucheza
kupoteza hamu ya kula na kushindwa kunyonya
Mtoto kubadilika rangi na kuwa na rangi bluu katika midomo na kucha
Hata hivyo, si lazima dalili zote hizi ziwepo kwa kila mtoto. Baadhi ya watoto huonesha kupumua kwa haraka kama dalili pekee ya homa ya mapafu. Iwapo vimelea vimeshambulia sehemu za chini ya mapafu karibu ya tumbo, sehemu ijulikanayo kama kiwambo au diaphragm, mtoto anaweza asioneshe hali yeyote ya kushindwa kupumua ingawa anaweza kuwa na homa na kujihisi maumivu makali ya tumbo, vichomi na pia kutapika.
Watoto wachanga wanaweza kushindwa kunyonya, na pia kupoteza fahamu na kupata degedege.

Vihatarishi vya homa ya mapafu (risk factors)
Katika hali ya kawaida kinga ya mtoto mwenye afya njema humlinda asishambuliwe na vimelea vinavyosababisha magonjwa mbalimbali. Hali huwa ni tofauti pale ambapo kinga ya mtoto ni ndogo au dhaifu, kwa vile mfumo mzima wa ulinzi huathirika na hivyo basi inakuwa ni rahisi kwa mtoto kupata homa ya mapafu.
Mfumo wa kinga wa mtoto unaweza kuwa dhaifu kwa ukosefu wa lishe bora hasa kwa watoto wachanga ambao hawanyonyeshwi ipasavyo. Aidha uwepo wa magonjwa mengine, kwa mfano, maambukizi ya VVU, saratani na ugonjwa wa Surua hupelekea kinga ya mwili kuwa dhaifu.
Lakini vile vile kuna mazingira yanayoweza kusababisha mtoto kuwa katika hatari ya kupata homa ya mapafu mfano moshi wa sigara, au moshi ndani ya nyumba unaosababishwa na kupikia kuni au mkaa. Vilevile msongamano ndani ya nyumba kutokana na watu kuwa wengi sehemu moja nayo huweza kusababisha watoto kupata homa ya mapafu.

Uchunguzi na Vipimo
Daktari humchunguza mtoto mgonjwa kwa kusikiliza dalili za ugonjwa kutoka kwa mzazi/mlezi wa mtoto, kuchunguza viashiria vya ugonjwa huu na kisha kumpima mtoto kwa kutumia kifaa kinachosaidia kusikia sauti mbalimbali katika mfumo wa hewa wa mgonjwa kiitwacho stethoscope.
Ili kujiridhisha na kuwa na uhakika wa tatizo hili, vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kulingana na mazingira na upatikanaji wake. Vipimo hivyo ni pamoja na X-ray ya kifua, au CT-scan ya kifua, pamoja na damu ili kuchunguza madhara yaliyoletwa na homa hii ya mapafu.
Faida ya kipimo cha CT-scan ni ule uwezo wake wa kutofautisha aina tofauti za homa ya mapafu na aina ijulikanayo kama Atypical pneumonia ambayo si rahisi kuonekana kwa kutumia X-ray ya kawaida ya kifua. X-ray ya kifua na CT-scan ya kifua kwa pamoja vina uwezo wa kuonesha tatizo hata pale ambapo daktari ameshindwa kusikia sauti maalum kwa kutumia kifaa chake cha stethoscope.

Matibabu
Maamuzi ya Matibabu kwa watoto wenye homa ya mapafu hutegemea aina ya vimelea, umri na hali ya mtoto. Mara nyingi antibiotics ndizo hutumika katika kutibu homa ya mapafu inayosababishwa na maambukizi ya bakteria. Kwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi, antibiotics hazina uwezo wowote wa kutibu. Ieleweke kuwa ni tabibu anayeweza kufahamu kama mtoto wako anahitaji antibiotics au dawa za aina nyingine, kwahiyo ni muhimu kwa mzazi ama mlezi kumpeleka mtoto hospitalini haraka pindi mtoto anapoonesha dalili za ugonjwa huu badala ya kuamua kumpa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

Namna ya kuzuia Homa ya mapafu
Homa ya mapafu inaweza kuzuiwa kwa chanjo, lishe bora na ya kutosha na mtoto kuishi katika mazingira yenye hewa safi.
Kuzuia homa ya mapafu kwa watoto ni sehemu muhimu ya mkakati wa Taifa wa kupunguza vifo vya watoto. Chanjo dhidi ya Hib, pneumococcus, surua na kifaduro ni njia mojawapo ya kuzuia homa ya mapafu.
Lishe ya kutosha ni muhimu kwa kuboresha kinga ya mwili ya mtoto ambapo inashauriwa mama kunyonyesha mtoto bila kuchanganya na kitu chochote walau kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha yake.
Kuhimiza usafi katika makazi kama kutotumia jiko la mkaa au kuni ndani ya nyumba na uvutaji wa sigara ni jambo linaloshauriwa pia. Hii inasaidia kupunguza idadi ya watoto kupata homa ya mapafu. Kwa watoto wenye VVU, matumizi ya dawa ya cotrimoxazole kila siku husaidia kupunguza uwezekano wa kupata homa ya mapafu.


Utafiti umeonyesha kwamba kinga na tiba sahihi ya homa ya mapafu inaweza kuzuia vifo milioni moja kwa watoto duniani kila mwaka. Hivyo ni wajibu wetu sote kushirikiana kupambana na ugonjwa huu wa homa ya mapafu.

ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOGU YETU...KARIBU TENA.
    Dr Theobard M.Rwiza.
Read more »


Friday, September 22, 2017

TATIZO LA MIMBA KUHARIBIKA NA VISABABISHI VYAKE


Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu wanawake wengi wamekuwa wakiharibikiwa na mimba bila kujua sababu.

Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba.

1.Mama anapokuwa na matatizo  uvimbe (fibroid),  huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara.

2. Uzito mkubwa (unene)

Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda.

3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara

Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika.

4. Utoaji mimba

Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba.

5. Matumizi ya Pombe,Sigara
Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo.

6. Magonjwa sugu
Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia.
Read more »


Friday, June 16, 2017

FAHAMU KULEGEA KWA MISULI YA UKE(VAGINAL PROLAPSE).

Tatizo hili huwatokea zaidi wanawake walio kaika umri mkubwa ingawa pia linaweza kutokea katika umri mdogo.Tunapozungumzia kulegea kwa misuli ya uke hapa kuna tofauti kidogo na kutanuka kwa misuli hiyo.Tukizungumzia kulegea ina maana misuli ya ukeni inashindwa kubcana na kuachia njia.Hapa misuli inayoachia njia inapolegea hata ukichuchumaa uhisi nyama zimejaa ukeni.

Chanzo cha tatizo
Kulegea kwa misuli ya uke kutokana na matatizo mbalimbali na hasa uzazi wa karibu karibu,mama anayezaa kwa vipindi viwili vifupi vifupi kwa njia ya kawaida hupatwa na tatizo hili,kulegea kutokana na matatizo ya vichocheo (Hormones) za kike,kulegea kunaweza kusababishwa na magonjwa sugu kama kansa,TB na maambukizi ya HIV,Magonjwa ya zinaa haswa kawende pia huchangia.

Kulegea kwa misuli ya uke kutokana na matatizo mbalimbali na hasa uzazi wa karibu karibu,mama anayezaa kwa vipindi viwili vifupi vifupi kwa njia ya kawaida hupatwa na tatizo hili,kulegea kutokana na matatizo ya vichocheo (Hormones) za kike,kulegea kunaweza kusababishwa na magonjwa sugu kama kansa,TB na maambukizi ya HIV,Magonjwa ya zinaa haswa kawende pia huchangia.

Mama anayeongezwa njia, baada ya uke kutanuka pia misuli pia inalegea,ingawa uke pia unaweza kutanuka hata bila hata ya misuli kulegea.Tatizo hili la kulegea misuli pia huchangiwa na umri mkubwa kwahiyo kwa wabibi hali hii inapojitokea ni kawaida hasa kuanzia umri wa miaka 70 na kuendelea.
                                                                      
Dalili za tatizo
Mama mwenye tatizo hili wakati wa kujisafisha ukeni atahisi kama tundu limeziba au limejaa nyama na inabodi atumie muda kujisafisha mara kwa mara atakuwa anasumbuliwa na muasho na uchafu wa mara kwa mara wakati wa kufanya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Mama mwenye tatizo hili wakati wa kujisafisha ukeni atahisi kama tundu limeziba au limejaa nyama na inabodi atumie muda kujisafisha mara kwa mara atakuwa anasumbuliwa na muasho na uchafu wa mara kwa mara wakati wa kufanya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Tatizo ambalo huambatana na uambukizo wa muda mrefu ukeni,pamoja na mama kutojisikia wakati wa tendo la ndoa,maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko,uambukizi huweza kupanda hadi kwenye mlango wa uzazi,tumbo la uzazi,mirija na vifuko vyo mayai.

Maambukizo yanapofikia huko mama huumwa na tumbo chini ya kitovu mara kwa mara,mwenendo wa siku za hedhi huvurugika kupata ujauzito.

Hali ya kulegea kwa misuli ya uke pia humuathiri hata mume kwani naye hushindwa kufurahia tendo la ndoa,kulegea na kutnuka kwa uke yote huathiri mahusiano ya kimapenzi kwani mama hafurahii na baba yake hafurahii tendo la ndoa.

Katika kutanuka kwa uke tumeona kuwa uke unatanuka zaidi ya kipenyo chake cha halali ambacho ni sentimeta nne,hivyohivyo kipenyo cha uume ni sentimeta nne.

Utawezaje kujua kama unatatizo? 
Mama mwenye tatizo la kutanuka kwa uke au kulegea kwa misuli ya uke anaweza kujigundua kwa kufuatilia dalili zote.Njia nyingine pitisha vodole viwili ukeni kama vitapwaya ongeza view vitatu vikiweza kuingia vitatu au zaidi bila shida yoyote sambamba na dalili ambazo tumekwisha ziona basi ujue unatatizo hili la kulegea kwa misuli ya uke inapolegea kama tulivyoona hapo awali utahisi kitu kinajaa au kuvimba au nyama zinajitokeza ukeni unapochuchumaa.

Mama mwenye tatizo la kutanuka kwa uke au kulegea kwa misuli ya uke anaweza kujigundua kwa kufuatilia dalili zote.Njia nyingine pitisha vodole viwili ukeni kama vitapwaya ongeza view vitatu vikiweza kuingia vitatu au zaidi bila shida yoyote sambamba na dalili ambazo tumekwisha ziona basi ujue unatatizo hili la kulegea kwa misuli ya uke inapolegea kama tulivyoona hapo awali utahisi kitu kinajaa au kuvimba au nyama zinajitokeza ukeni unapochuchumaa.

Uchunguzi
Muone daktari wa magonjwa ya akina mama kwa uchunguzi na ushauri wa tiba.Vipimo mbalimbali vitafanyika kubainisha tatizo kama kipimo cha damu,vipimo vya ukeni mfano kipimo cha speculum examination,kuotesha uchafu wa ukeni,kama mama ana maumivu ya tumbo vipimo vya ultrasound pia vitafanyika,mwenendo wa mfumo homoni na historia ya tatizo kwa ujumla itafanyiwa tathimini,vilevile itasaidia kujua kama tatizo ni la kuzaliwa nalo,uzazi wa karibu karibu au ni nini.Uchunguzi huu ufanyika ili kuweza kupanga tiba ambayo huwa zaidi ya umoja ili kuweza kufanikisha.

Muone daktari wa magonjwa ya akina mama kwa uchunguzi na ushauri wa tiba.Vipimo mbalimbali vitafanyika kubainisha tatizo kama kipimo cha damu,vipimo vya ukeni mfano kipimo cha speculum examination,kuotesha uchafu wa ukeni,kama mama ana maumivu ya tumbo vipimo vya ultrasound pia vitafanyika,mwenendo wa mfumo homoni na historia ya tatizo kwa ujumla itafanyiwa tathimini,vilevile itasaidia kujua kama tatizo ni la kuzaliwa nalo,uzazi wa karibu karibu au ni nini.Uchunguzi huu ufanyika ili kuweza kupanga tiba ambayo huwa zaidi ya umoja ili kuweza kufanikisha.

Matibabu na ushauri
Tiba hutolewa katika Hospitali kubwa au katika cliniki maalum za magonjwa ya akinamama,tiba ni kurekebisha misuli hiyo kwa njia ya upasuaji mdogo na baadhi ya dawa ili kumrudisha mama katika hali ya kawaida.

Mwanamke aepuke vyanzo mbalimbali mojawapo ni uzazi wa karibu karibu hivyo afuate uzazi wa mpango uwe wa kalenda,sindano,vidole au vijiti au kitanzi.

Tiba hutolewa katika Hospitali kubwa au katika cliniki maalum za magonjwa ya akinamama,tiba ni kurekebisha misuli hiyo kwa njia ya upasuaji mdogo na baadhi ya dawa ili kumrudisha mama katika hali ya kawaida.Mwanamke aepuke vyanzo mbalimbali mojawapo ni uzazi wa karibu karibu hivyo afuate uzazi wa mpango uwe wa kalenda,sindano,vidole au vijiti au kitanzi.

Epuka kupata magonjwa au maradhi ya ukeni mara kwa mara kwa kujisafisha vizuri na unapohisi tu unatatizo ukeni haraka muone daktari anayeshugulika na magonjwa ya kinamama kwa msaada mkubwa.

Chakula bora hasa mboga za majani na matunda mara kwa mara kwa kulinda na kuimarisha mwili mojawapo ni kuweka sawa mwenendo wa mfumo wa homoni kuimarisha muonekano wa mwili na viungo vya uzazi na upevushaji wa mayai.Wahi hospitali kwa uchunguzi.



ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOGU YETU....KARIBU TENA.
Read more »


JE, WAJUA KUWA SIGARA HUHARIBU DNA MWILINI NA KUONGEZA HATARI YA KUPATA KENSA???BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI


Kemikali za sumu zilizoko katika tumbaku ya sigara huharibu DNA za mwili wa binadamu dakika chache tu baada ya mtu kuanza kuvuta sigara. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, kemikali hizo zinazoitwa Polycylic Aromatic Hydrocarbons (PAHs) husababisha DNA ziharibike na kuongeza uwezekano wa mtu kupata kensa. 

Katika uchunguzi huo watalamu walichukua kemikali hizo katika miili ya wavuta sigara na kuzifanyia uchunguzi, ambapo waligundua kuwa, kemikali za PHA hubadilika haraka mwilini na kuwa sumu ambayo huharibu DNA baada ya kupita dakika 15 hadi 30 tangu kuingia tumbaku katika mwili wa binadamu. Sumu hiyo hubadilisha seli mwilini au kufanya mutation, kitendo ambacho huweza kusababisha kensa. Wataalamu hao wanasema, kitendo hicho hufanyika kwa haraka sana kama vile inavyoingizwa mada ya sumu kwenye damu kwa sindano. 

Habari hii ni tahadhari kwa watu wanaotaka kuanza kuvuta sigara, kwani takwimu zinatuonyesha kwamba, watu 3,000 hufariki dunia kila siku umwenguni kutokana na kensa ya mapafu, maradhi ambayo husababishwa kwa asilimia 90 na uvutaji sigara. Madhara ya kuvuta sigara kwa muda mrefu yanajulikana na wengi, ambayo ni pamoja na magonjwa ya moyo na kensa mbalimbali, lakini wataalamu wanatuasa ya kuwa, madhara ya sigara huanza pale tu mtu anapoanza kupiga pafu ya kwanza na kuingiza moshi wa sigara mwilini. Hivyo bado hujachelewa na unaweza kuacha sigara hii leo!
Read more »


Thursday, June 15, 2017

FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KUKOSA CHOO KWA WATOTO WADOGO AU KUWA NA CHOO KIGUMU NA JINSI YA KULITATUA



Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua

Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation. Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.

Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.

Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.

2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.

3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.

4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.

5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.

6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.

7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng’ombe.

8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi.

N.B Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.

Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.

Read more »