Ugonjwa huu huambukizwa kwa mtu kula au kunywa chakula au maji yalio na kinyesi cha mtu aliyambukizwa.
Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu.
Je? Dalili za homa ya matumbo ni zipi?
- Homa kali
- Kutoka kwa majasho mengi
- Kuharisha (bila ya kutoa damu)
- Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
Katika wiki ya kwanza:
- Joto la mwili huongezeka
- Kichwa huuma
- Kukohoa
- Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
- Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Katika wiki ya pili:
- Homa huongezeka
- Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
- Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
- Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
- Kutapika kwa mgonjwa
- Ini la mgonjwa huvimba
- Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu:
- Matumbo hutoa damu.
- Matumbo hutoboka
Wiki ya tatu ikimalizika, homa huanza`kutulia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.
Matibabu ya homa ya matumbo yapi?
Kumbuka: Homa ya matumbo haiuwi binadamu. Ila pindi uonapo kati ya dalili zilizoainishwa hapo juu ni vema ukawahi Tiba na vipimo sahihi vya kitaalamu katika kituo cha afya kilicho karibu na wewe.
Ni Jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya matumbo?
- Usafi wa mazingara na wa kibinafsi ni hatua bora ya kujikinga kutokana na ugonjwa huu.
- Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hivyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
- Homa hii hueza kuenea kwenye mazingara ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kinga bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
- Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayoTy21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Viiliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.
ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOGU YETU....KARIBU TENA.
Dr. Theobard M.Rwiza.
No comments:
Post a Comment