Tuesday, August 16, 2016

UGONJWA WA SELI MUNDU(SICKLE CELL): FAHAMU ASILI YAKE,DALILI,VIPIMO VYA KITABIBU NA MATIBABU YAKE..


Ugonjwa wa sickle seli ni mojawapo ya magonjwa yakurithi yanayoathiri mwanadamu. Ugonjwa huu unarithiwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Tatizo hili linaathiri damu. Molekyuli inayoathiriwa ni HAEMOGLOBIN
 Haemoglobin ni sehemu ya chembe hai nyekundu zilizoko damu.Kazi yake ni  kuzisaidia chembe hai nyekundu kubeba hewa ya oksijenu kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu nyingine za mwili.

Kwa kawaida binadamu anapozaliwa huwa na himoglobini A (HbA) na Himoglobini ya kichanga Himoglobini F (HbF).
Chembe hai nyekundu za damu za kawaida huwa laini,za duara na huweza kujipenyeza katika mishipa ya damu kirahisi.Pia huweza kuishi kwa takriban siku mia moja na ishirini (120) kisha huaribiwa. Mgonjwa wa  sickle cell  huwa na chembe hai nyekundu ngumu, zenye umbo la mundu  ambazo hupita kwa taabu kwenye mishipa ya damu haswa ile midogo.Aina hii ya himoglobini huitwa Himoglobini S (HbS).
Tofauti na chembe hai nyekundu za damu za kawaida,zenyewe huishi kwa siku chache zaidi.

Kwa hiyo ugonjwa wa sickle cell ni ugonjwa wa kurithi ambapo mwathirika huwa na himoglobini S.Hali hii hupelekea kuwa na upungufu wa damu kwenye baadhi ya sehemu mwilini.
Iwapo chembe hai nyekundu za damu  zenye HbA ni zaidi ya HbS huweza kutengeneza HbAS.Hali hii hujulikana Sickle Cell Trait maana mwathirika hana dalili zozote.Mara nyingi watu hawa huishi maisha ya kawaidahii.
Ugonjwa wa sickle cell ni ugonjwa   wa kudumu..Umri wa kuishi hupungua na baadhi ya tafiti za nyuma zinaonyesha kwamba waweza kuishi kwa wastani wa miaka arobaini (40) mpaka hamsini (50).Waafrika wengi hasa kusini mwa jangwa la sahara huathiriwa zaidi na tatizo hili.

Katika mazingira yenye kiwango kidogo cha oksijeni, chembe hai nyekundu za damu zenye umbo la kawaida (mviringo) huharibiwa na kupoteza uwezo wa kutanuka na kusinyaa (elasticity) zipitapo kwenye mishipa ya damu.Hali hii hupelekea chembe hai hizo nyekundu za damu kuharibiwa na mfumo wa damu kwenye bandama (spleen) Pia hupelekea kuziba kwa mishipa midogo ya damu. Hali hii inaweza kusababisha kukosekana kwa damu na oksijeni ya kutosha katika baadhi ya viungo.
Dalili za sickle cell
Katika miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa  dalili hujitokea mara chache.Hii inatokana na kuwepo kwa wingi kwa himoglobini F, ambayo huzilinda chembe hai.

Dalili utotoni 

-Maumivu ya viungo vya mikono na miguu
-Kushambuliwa na maradhi kama hom ya uti wa mgongo, homa ya mapafu  na mafua
-Kuvimba kwa bandama kutokana na kujaa ghafla kwa damu kwenye bandama 
-Kusinyaa kwa bandama(autosplenectomy)

Dalili ukubwani

-Upungufu wa damu 
-Maumivu ya tumbo 
-Maumivu ya mifupa na viungo
-Kupooza
-Maumivu ya kifua kama homa ya mapafu (acute chest syndrome) 
-kupumua kwa taabau 
-Kukojoa damu 
-Vidonda ndugu(chronic ulcers) miguuni 
-Kusimama kwa uume kuambatanako na maumivu makali (priapism) 
-Kuvimba kwa paji la uso au fuvu

 Uchunguzi

Vipimo vifuatavyo ni muhimu katika kugundua sickle cell na magonjwa yaambatanayo na sickle cell;

-Sickling Test
-Kipimo cha  Malaria 
-Kipimo cha mkojo(urinalisis 
-Picha ya kifua (x-ray) kuangalia iwapo kuna athari katika kifua 
-Kipimo cha wingi wa damu (Hb level)

Matibabu

Aina ya matibabu  hutegemeana na aina ya mgonjwa na tatizo linalomsumbua kwa wakati huo.
Hivyo mgonjwa anaweza kutumia dawa za aina tofauti ikiwemo dawa za maumivu, antibiotik, kuongezwa maji na hata wakati mwingine kuongezewa damu.

KUMBUKA: itaendelea wiki ijayo....endelea kufatilia hapahapa TABIBU WA KWELI.

ASANTE SANA KUTEMBELEA BLOGU YETU...KARIBU TENA.
  Dr Theobard M.Rwiza.

No comments:

Post a Comment